Mudavadi asema mazungumzo ya NASA kuzingatia katiba ya sasa

Mudavadi asema mazungumzo ya NASA kuzingatia katiba ya sasa

Kinara wa Amani National Congress Musalia Dudavadi sasa amesisitiza kuwa makubaliano ya uongozi katika muungano wa nasa yatazingatia katiba iliyoko kwa sasa, ambayo ni bayana kuhusu nafasi za uongozi zinazotambulika kikatiba.
Mudavadi anawataka wakenya kuwa na subra huku mjadala wa kumchagua atakayetoana kijasho na rais huru Kenyatta Agosti ane ukielekea kumalizika.
Haya yanajiri huku rais Uhuru Kenyatta akifanya kikao na rais mstaafu Daniel Moi katika kile wadadisi wanakitaja kama kusaka mawaidha kuambatana na uchaguzi mkuu ujao, chini ya mwezi mmoja baada ya Mama Ngina Kenyatta kumtembelea rais huyo mstaafu nyumbani Kabarak.

Also read:   Uganda na Kenya kushirikiana kuimairisha usalama Migingo

Related stories