Gavana Joho adokeza hahitaji ulinzi kutoka kwa serikali

Gavana Joho adokeza hahitaji ulinzi kutoka kwa serikali

Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho kwa mara nyingine ameshambulia serikali ya Jubilee wakati huu kuhusiana na mzozo wa kuondolewa kwa walinzi wake akisema hana haja ya ulinzi wa serikali akisema mlinzi wake mkuu ni maulana na wananchi anaowatumikia.
Haya yanajiri huku mshirikishi wa eneo la Pwani Nelson Marwa akionya wale wanaomiliki bunduki kinyume cha sheria katika eneo la Pwani kuzisalimisha bunduki hizo kabla serikali haijachukua hatua dhidi yao.
Hapo jana seneta wa kaunti hiyo Hassan Omar Hassan aliitaka serikali kuchunguza uhalali wa bunduki zinazomilikiwa na Joho na familia yake.

Also read:   Wafanyikazi Wa Shirika La CDA Waandamana Mombasa.

Related posts

MNL App
MNL App