HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosUS Election 2016

Trump auchachawiza ulimwengu kwa kushinda uchaguzi wa Marekani

Ulimwengu mzima ungali unajaribu kung’amua ushindi wa Donald Trump ambaye sasa ndiye rais mteule wa Marekani, kufuatia uchaguzi ambao bila shaka utakumbukwa kwa miaka mingi. Trump alimshinda mpinzani wake wa chama cha Democrats bi. Hillary Clinton kwa wingi wa kura za kura za waakilishi, kumwezesha kuingia ikulu ka kura 289 dhidi ya 218 alizozoa Clinton, lakini Clinton akashinda kwa wingi wa kura za kitaifa, kinyume na matarajio ya wengi. Trump alimpongeza Clinton kwa kampeni alizoendesha na kusema Marekani inastahili kumheshimu Clinton huku Clinton akimpongeza Trump kwa kutwaa ushindi. Rais Obama amemwalika Trump Alhamisi, 10 Novemba, kwa kikao katika ikulu ya White House kujadili masuala ya mpito.

Show More

Related Articles