HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Rais Kenyatta asubiriwa kuamua suala telezi la riba iwapo kutakuwa na udhibiti

Tangu mjadala kuhusu sheria ya kuweka kiwango cha juu zaidi cha riba inayostahili kutozwa wateja na benki isizidi asilimia nne juu ya kiwango cha riba kilichopendekezwa na Benki Kuu, benki nane zimepunguza kiasi cha riba , katika harakati za kuwaridhisha wateja wake .
Rais Uhuru Kenyatta ambaye ana siku 14 za kuweka sahihi sheria kuhusu riba ana kibarua cha kufanya uamuzi wa kufa kupona, wa kuweka sahihi sheria hiyo na kuwaridhisha wananchi , au kukataa kuitia sahihi , kama alivyopewa mawaidha na wakuu wa serikali wanaosimamia masuala ya uchumi.

Show More

Related Articles