HabariMilele FmSwahili

Wizara ya elimu kuchunguza kozi 100 katika vyuo vikuu nchini

Imebainika zaidi ya kozi 100 katika vyou vikuu nchini hazijachakuliwa na wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo mwaka huu. Kutoka na hali hii waziri wa elimu profesa George Magoha ameagiza uchunguzi wa kozi zote akihidi kufutilia zile zitazopatikana bila manufaa yoyote kwa wanafunzi.

Akungumza katika hafla ya uteuzi wa wanafunzi, mwenyekiti wa kituo cha kuwapa nafasi wanafunzi hao Joe Osaka naye ameitaka bodi ya ufadhili wa masomo ya juu nchini Helb kutochelewesha ufadhili huo kwa wanafunzi

Mwaka huu wanafunzi 89,486 watajiunga na vyuo vikuu ikilinganishwa na idadi ya hapo awali ya wanafunzi 90,755. Hii ni baada ya wanafunzi 1269 kati yao kuamua kujiunga na taasisi za kiufundi.

Show More

Related Articles