Mediamax Network Limited

Serikali Yaanzisha Rasmi Ugavi Wa Chakula Kaunti Ya Kwale.

Waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa hii leo amekita kambi eneo la kinango kaunti ya kwale kuongoza zoezi la ugavi wa chakula kwa wale wanaoathirika na njaa eneo hilo.

Akiongea wakati wa zoezi hilo gavana wa kwale Salim Mvurya amewapa hakikisho wenyeji kwamba shughuli hiyo, itaendelezwa katika sehemu zote zinazokabiliwa na ukame ikiwemo Kinango, Matuga na Msambweni kuona kuwa hakuna mtu atakaefariki kutokana na njaa.

Mapema leo wenyeji  wameiomba serikali kuongeza vipimo vya chakula wanachopewa, sawia na kuwawekea mikakati ya kupata maji safi ya kunywa kutokana na mahangaiko wanayopitia, wakisema kilo 2 hadi 3 wanazopewa hazitoshi. Hali hiyo imethibitishwa na naibu kamishna wa eneo la Gulanze Mike Nakure ambaye anasema endapo mikakati ya kutosha haitawekwa kusaidia wakazi huenda hali ikazidi kuwa mbaya zaidi. Ripoti zinaeleza kuwa zaidi ya watu 120000 wamo kwenye hatari ya kuathirika na ukame katika kaunti hiyo.