HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Mwalimu Kutoka Kenya Aibuka Bora Zaidi Duniani.

Mwalimu wa sayansi kutoka shule ya Upili ya Kericho kaunti ya Nakuru  , ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi maskini zaidi , ameshinda tuzo la dola milioni moja $1m  ambayo ni sawa na shilingi milioni 100 kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani.

Peter Tabichi, ambaye anatoka katika shirika la kidini la Francisco , alishinda tuzo la dunia la mwaka 2019 la mwalimu bora wa sayansi na hisabati.

Peter amesifiwa kwa mafanikio yake katika shule yenye madarasa yenye watoto wengi pamoja na vitabu vichache. Anataka kuwaona watoto wa shule kuiona “sayansi kama njia ya kufuata ” kwa ajili ya siku zao zijazo.

Show More

Related Articles