HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Uhaba Wa Maji Washuhudiwa Mombasa Kwa Zaidi ya Miezi 3.

Uhaba wa maji unaendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbali za miji ya mombasa, Kilifi na Kwale.

Hali hiyo imetajwa kutokana na kuharibika kwa bomba kuu linalotoa maji kutoka chemichemi ya mzima kaunti ya Taita-taveta. Maelfu ya wakazi wa changamwe , KIBARANI na Jomvu ndio walioathirika zaidi, huki baadhi yao wakisalia bila maji kwa zaidi ya miezi mitatu.

Wengi wameitaka serikali na idara husika kushughulikia tatizo hilo ili kuwaondolea dhiki ya kupata maji. Kulingana na baadhi Bei ya maji imepanda kutoka shilingi mbili 2 na 5 kwa kila mtungi moja, hadi shilingi 30 na 50 hali ambayo wanahofia huenda ikawazidishia ugumu wa maisha hata zaidi.

Sehemu nyingine zilizotajwa kuathirika na uhaba wa maji ni kaunti za kilifi na Kwale.

Show More

Related Articles