HabariPilipili FmPilipili FM News

Akaunti Za Mitandao Ya Kijamii Za Rais Kenyatta Zafungwa.

Akaunti za mitandai ya kijamii za rais Uhuru Kenyatta zimefungwa baada ya kusemekana kwamba zimedukuliwa na watu ambao hawajaidhinishwa.

Mkuu wa wafanyikazi katika afisi ya rais NZIOKA WAITA, amesema akaunti zote za rais za Twitter na Facebook zimefungwa kwa sasa ili ziweze kurekebishwa.

Chapisho la mwisho kwenye akaunti yake ya Twitter, rais alishinikiza kwamba hatamsaza yeyote katika vita dhidi ya ufisadi hata kama ni ndugu yake au mwandani wake wa karibu wa kisiasa.

 

 

 

Show More

Related Articles