HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Wanaoishi Nje Ya Nchi Kupewa Stakabadhi Za Usafiri Kwenye Nchi Wanazoishi.

Rais Uhuru Kenyatta ameaumuru idara ya uhamiaji kuwapatia wakenya wanaoishi nje ya nchi paspoti za sasa.

Ametaka wakenya hao popote wanapoishi nje ya taifa hili wapewa paspoti hizo haraka.

Akiongea katika ziara yake nchini Namibia rais Kenyatta ametoa agizo hilo alipokutana na wakenya ambao wanaishi na kufanya kazi mataifa ya Afrika Kusini.

Amesema haoni umuhimu wa wakenya hao kusafiri hadi Nairobi kutuma maombi ya paspoti hizo.

Show More

Related Articles