HabariPilipili FmPilipili FM News

Toufiq Balala Matatani Mombasa.

Kivumbi kinatrarajiwa adhuhuri hii leo katika bunge la kaunti ya Mombasa ambapo wabunge wa kaunti wanatarajiwa kujadili hoja ya kutokuwa na imani na waziri wa uchukuzi  wa kaunti Toufiq Balala.

Wabunge hao wanatilia shaka utendakazi wa waziri huyo wakisema hajakuwa akitekeleza majukumu yake ipasavyo.

Wanasema wizara yake imekuwa ikipokea mamilioni ya pesa kila mwaka kutoka kwa serikali ila pesa hizo hazijafaidisha wenyeji wa kaunti ya Mombasa.Pia wanamshtumu Balala kwa kususia kufika mbele ya bunge la kaunti  kujibu masuali kuhusu masuala ibbuka.

Jumla ya wawakilishi wadi 38 kati ya 42 wametia saini hoja ya kutokuwa na imani na uongozi wa waziri huyo.

Haya yanajiri wakati baadhi ya wawakilishi wadi wakitarajiwa kufika mbele ya kamati ya chama cha ODM hii leo.

Hata hivyo wawakilishi hao wamelaumu hatua ya chama hicho kuita baadhi ya wawakilishi wadi, wakisema hatua hii haionyeshi usawa.

 

Show More

Related Articles