HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Noordin Hajji Awaonya Wanaokiuka Haki Za Wananchi Lamu.

Mkurugeniz wa mashtaka ya umma Noordin Hajji amewapa hakikisho wakazi wa lamu waliopata mateso mikononi mwa polisi katika kaunti hiyo  kwamba watapata haki. Hajji pia amewapa hakikisho la kupata haki wanaokabiliwa na matatizo ya ardhi ndani ya kaunti hiyo.

Akizungumza na wakazi eneo la Mkunguni mjini Lamu alipofungua rasmi kituo cha haki na usawa , Hajji amesema atahakikisha wale wanaokiuka haki za wanachi wanachukuliwa hatua zifaazo kisheria.WENGI wamelalamikia kunyanyaswa na maafisa wa polisi, wakihusisha baadhi ya maafisa hao kwa ufisadi wakati wa kuhudumia wananchi.

Show More

Related Articles