K24 TvNEWSSwahiliVideos

KIFO CHA DAKTARI CUBA: Familia yasema alikuwa amelalamikia maisha magumu.

Serikali ya Kenya pamoja na serikali ya Cuba zimeanzisha uchunguzi kufuatia kisa cha mmoja wa madaktari kutoka Kenya kufariki katika hali tatanishi jijini Havana, Cuba.

Marehemu, Daktari Hamisi Ali Juma, ambaye pia ni nduguye Mbunge wa Likoni, Bi. Mishi Mboko, anaripotiwa kulalamikia familia yake kwamba alitaka arejeshwe nyumbani akidai maisha nchini Cuba yalikuwa magumu mno kuambatana na mazingira na kipato kidogo walichokuwa wakitegemea kutoka kwa serikali.

Show More

Related Articles