HabariPilipili FmPilipili FM News

Idadi Ya Waliofariki Kwenye Shambulio La NewZealand Yafikia 49.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, kamishna wa polisi Mike Bush anasema, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali. Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Show More

Related Articles