HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Samboja Ataka Madaktari Wanaolemaza Huduma Taita Kuchunguzwa.

Madaktari wanachunguzwa kauti ya Taita-taveta kwa kile kimetajwa wao kulemaza huduma katika hospitali na vituo vya afya vya kaunti hiyo.

Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja anasema  baadhi ya madaktari katika hospitali za umma wamekuwa wakificha dawa , na wengine kuomba shilingi 200 hadi mia 500 kwa wagonjwa ili kutoa dawa pamoja na kuuza bidhaa nyingine za hospitali.

Samboja ameonyesha kusikitishwa kwake  na kukosekana kwa dawa katika hospitali za umma licha ya fedha nyingi zinazowekezwa katika sekta hiyo.

Hata hivyo usimamzi wa hospitali ya rufaa mjini Voi umetaja ukosefu wa usalama wa kutosha  katika hifadhi za za dawa ndani ya kaunti hiyo kuwa unachangia wizi wa dawa hizo.

 

Show More

Related Articles