HabariPilipili FmPilipili FM News

Profesa Magoha Apigwa Msasa Na Bunge Kuhusu Uteuzi Wake Kama Waziri Wa Elimu.

Profesa George Magoha hii leo amefika Mbele ya kamati ya bunge kupigwa msasa kuhusu uteuzi wake kuongoza wizara ya elimu; profesa Magoha alitakiwa kujieleza kuhusiana na TAALUMA yake, MASOMO na hata historia ya utendakazi wake, kubaini iwapo anatosha kuongoza wizara ya elimu nchini au la.

Maghoha ambaye anachukua wadhfa huo kutoka kwa balozi Amina Mohamed aliehamishiwa kwa wizara ya michezo, amepuuza tuhuma za baadhi ya wabunge kwamba uongozi wake ni wa kidikteta, akisema yeye ni mchapakazi muadilifu.

Kamati hiyo ina hadi Machi 19 kuidhinisha au kukataa uteuzi wa profesa George Magoha.

Iwapo profesa Magoha ataidhinishwa atakua na kibarua cha kufanikisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu, sawia  na kuafikia usajili wa asilimia 100 ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili.

Show More

Related Articles