HabariMilele FmSwahili

Profesa Magoha atetea tajiriba yake kama waziri wa elimu

Profesa Magoha ametetea uteuzi wake kama waziri wa elimu akitaja tajiriba yake na uzoefu anaosema utamwezesha kutekeleza majikumu ya waziri wa elimu. Profesa Magoha pia ameapa kutekeleza mabadiliko ya busara katika wizara. Akipigwa msasa na kamati ya bunge ya uteizi Magoha amesema anaunga mkono mtaala mpya wa elimu huku akisema atahakikisha kufikia mwezi Agosti, mtaala huo unatekelezwa kikamilifu iwapo ataidhinishwa na bunge.

Pia ameahidi kukabiliana na visa vya dhuluma za kijinsia na mimba za mapema kwa wanafunzi. Magoha amesisitiza iwapo ataidhinishwa, wahusika katika mienendo hiyo watakiona chamtemakuni.

Magoha pia amekana kuegemea upande wowote wa kisiasa na kujitenga na swala la ukabila ambapo amesema hilo halijashuhudiwa popote katika utendakazi wake wote.

Sasa bunge linatarajiwa kutoa uamuzi wake ambapo iwapo litamuidhinisha basi magoha atachukua mahali pake aliyekuwa waziri wa elimu balozi Amina Mohamed ambaye alipewa uhamisho hadi wizara ya michezo.

Show More

Related Articles