HabariMilele FmSwahili

Waziri mteule wa elimu George Magoha kupigwa msasa na kamati ya bunge leo

Waziri mteule wa elimu profesa George Magoha atapigwa msasa leo na wabunge kufuatia uteuzi wake kutwaa nafasi ya balozi Amina Mohamed. Profesa Magoha ameratibiwa kufika mbele ya kamati ya bunge ya uteuzi inayoongozwa na spika Justine Muturi saa nne asubuhi. Kamati hiyo inahadi Machi 19 kuidhinisha au kukataa uteuzi wa profesa Magoha. iwapo ataidhinishwa profesa Magoha atakabiliwa na kibarua cha kufanikisha utekelezaji wa mtaala mptya wa elimu na mchakato wa kuhakikisha kuwa asilimia 100 ya wanafunzi wanaomaliza darasa la nane wanajiunga na shule za upili.

Show More

Related Articles