HabariPilipili FmPilipili FM News

Visa Vya Kuwanyanyasa Wanahabari Vyakithiri Kwale.

Visa vya wanahabri  kudhalilishwa na kutishiwa maisha   katika afisi za serikali kaunti ya Kwale, vinahofiwa kuongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Mwanahabari wa shirika la KENYA NEWS AGENCY Kwale ni wa hivi punde kudhalilishwa ,baada ya kuzuru afisi ya waziri wa afya katika kaunti hiyo Francis Gwama ,kutafuta  habari za ufunguzi wa  chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Kwale.

Shaban Omar anasema juhudi zake za kupata  habari hizo ziliambulia patupu baada ya kutimuliwa kutoka afisi hiyo na Gwama.

Mwanahabari huyo  sasa anamtaka gavana wa kaunti yak wale Salim Mvurya kuainisha  uongozi wa wizara katika kaunti hio, kuona kuwa wanahabari na wakaazi  wanapata habari  muhimu wanazohitaji kutoka kwa afisi ya serikali.

Katika kisa tofauti wanahabari wanne walinyimwa habari pale walipotembelea afisi ya Ushuru baada ya mkurgenzi wa ofisi hiyo kuwataka kuomba ruhusa mumewe kabla ya kuwapatia taarifa walizohitaji.

Show More

Related Articles