HabariPilipili FmPilipili FM News

Ziara Ya Macron Nchini Yaleta Mazuri.

Kenya na Ufaransa inatarajiwa kushirikiana kwa kutia saini miradi mbalimbali ya maendeleo humu nchini.

Kwenye taarifa ya pamoja na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta, rais wa ufaransa Emmanuel Macron amedhibitisha kuwa serikali yake itafungua viwanda vya utengenezaji magari miongoni mwa viwanda vyengine.

Aidha Macron amesema Kenya ina nafasi nzuri ya kujiinua kimaendeleo kwani wawekezaji  kutoka taifa lake watakuwa ni wenye kuwekeza kwa wingi humu nchini.

Kwa upande wake rais Uhuru Kenyatta  ameipongeza serikali ya ufaransa kwa kuwekeza humu nchini na kusema tayari kiwanda cha kutengeneza magari ya peageot kimewaajiri vijana wengi na kusema aina ya magari hayo ni mazuri kwani hayatumii mafuta mengi ikilinganishwa na magari mengine.

 

Show More

Related Articles