HabariPilipili FmPilipili FM News

Hajj,Kinoti Na Mbarak Waapa Kupambana Na Ufisadi.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajj,Mkurugenzi wa DCI George Kinoti na afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak wamefika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye bunge la seneti kuelezea hatua walizopiga katika kupambana na ufisadi.

Hajj na Kinoti wamekiri kuwa kumekuwa na ubadhirifu wa mali ya umma katika kaunti nyingi huku wakiahidi kuzidisha juhudi za kuwakabili wahusika.

Hajj ameomba kupewa muda zaidi kukamilisha uchunguzi kuhusiana na kupotea kwa mabilioni ya pesa katika ujenzi wa mabwa ya Aror nakimwarer.

Wote hao wameambia kamati ya seneti kwamba wameweka mikakati ya kuwanasa wanaotoa stakabadhi bandia mahakamani , na kuwachukulia hatua kali kisheria.

Show More

Related Articles