HabariMilele FmSwahili

Watu wawili waangamia kutokana na makali ya ukame Turkana

Watu wawili wameangamia kutokana na athari za ukame katika kaunti ya Turkana. Mwili wa mwanamke mmoja umepatikana katika kijiji cha Kang’irasai Turkana ya kati huku wenyeji wakisema mtu mwengine mmoja amefariki katika kijiji hicho. Kulingana na chifu wa eneo hilo John Ekwar wenyeji ambao pia  wamepoteza mifugo kadhaa waliokufa kutokana na ukosefu wa lishe na maji. Mbunge wa Turkana ya kati Jonh Lodepe na waziri wa maji kaunti ya Turkana Emathe Namwar wameitaka serikali na wahisani kuwasaidia wakazi wanaotaabika kutokana na eneo hilo kutoshuhudia mvua katika mwaka mmoja uliopita.

Show More

Related Articles