HabariPilipili FmPilipili FM News

Ipeni Nafasi DCI Ifanye Kazi Yake Asema Chonga.

Viongozi wa kisiasa wanapaswa kuipa nafasi idara ya upelelezi wa jinai DCI kukamilisha uchunguzi wake kuhusiana na sakata ya shilingi bilioni 21 zinazodaiwa kufujwa kwenye miradi ya mabwawa ya Arorr Na Kimwarer kaunti ya Elgeiyo Marakwet.

Hiyo ni kauli ya Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga , ambaye ameeleza kushangazwa na hatua ya naibu rais Wiliam Ruto hivi majuzi alipokanusha kiwango cha fedha kinachodaiwa kupotea , pale alisema ni shilingi bilioni 7 pekee zinazopaswa kuchunguzwa.

Chonga amezitaka idara husika kufanya uchunguzi wa kina akisema ufisadi ndio changamoto kuu inayoathiri uchumi wa taifa hili.

Show More

Related Articles