HabariMilele FmSwahili

Wakongwe kupokea pesa za kujikimu wiki ijayo, mfumo mpya wa usambazaji ukuzinduliwa

Wakongwe, mayatima na watu wenye changamoto ya ulemavu ambao hawajakuwa wakipokea pesa za kujikimu kutoka kwa serikali kipindi cha miezi sita iliyopita sasa watazipokea kuanzia jumatatu ijayo. Hii ni baada ya serikali kuzindua mfumo mpya wa kusambaza pesa hizo kupitia akaunti za benki. Mark Botongore ni naibu mkurugenzi kitengo cha masuala ya jamii ambacho kinasimamia usambazaji wa fedha hizo.

Hata hivyo anasema wale ambao bado hawajafungua akaunti wana nafasi ya kuendelea kufanya hivyo. Amewahakikishia watapokea fedha zao.

Katibu katika wizara ya ugatuzi Nelson Marwa anasema hatua hii inalenga kupambana na ufisadi wakati wa kutolewa kwa pesa hizo.

Show More

Related Articles