HabariMilele FmSwahili

Jaji Joseph Mutava asimamishwa kazi

Jaji Joseph Mutava amesimamishwa kazi. Hii ni baada ya mahakama ya upeo kuridhia mapendekezo ya jopo lililomchunguza na kumpata na hatia ya kukiuka maadili ya kazi. Majaji wa mahakama hiyo wanasema kulikua na sababu za kutosha kumtimua kazini jaji huyo. Jaji Mutava alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa jopo hilo kwa dai, lalama zote kuhusu madai yaliyokuwa yakimkabili yalikuwa yameondolewa.Jopo hilo lililoongozwa na jaji mkuu David Maraga liliagiza aondoke afisini kufuatia maamuzi yake kama jaji ikiwemo ile kesi ya Goldenberg ambapo taifa lilipoteza kiwango kikubwa cha fedha. Jumla ya mashahidi 29 walifika mbele ya jopo hilo.Mutava likuwa akikabiliwa na madai sita  ambayo jopo hilo liliyathibitisha.

Show More

Related Articles