HabariPilipili FmPilipili FM News

Bunge Kujadili Kuhusu Ripoti Ya Uhasibu.

Bunge la kitaifa adhuhuri ya leo linatarajiwa kujadili ripoti ya kamati ya uhasibu bungeni kuhusiana na taarifa ya kifedha ya mwaka 2017 – 2018 kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Wabunge wanatarajiwa kujadili mapendekezo ya kamati hiyo kwamba makamishna wa IEBC wanafaa kupigwa kalamu kufuatia usimamizi mbaya wa afisi hiyo chini ya uongozi wa mwenyekiti wake Wafula Chebukati.

Kamati hiyo inayoongozwa na Opiyo Wandayi imekuwa ikichunguza vitabu fedha vya IEBC kwa takriban miezi mitatu sasa na sasa inashinikiza kuondolwa madarakani kwa Chebukati pamoja na makamishna Boya Molu na Abdi Guliye.

 

Show More

Related Articles