HabariPilipili FmPilipili FM News

Raila Azidi Kuunga Mkono Kufanyiwa Marekebisho Kwa Katiba.

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesistiza ipo haja ya kufanyiwa marekebisho katiba ya humu nchini.

Akiongea kwenye mahojiano na redio moja humu nchini Raila amewataja wanaopinga marekebisho ya katiba kuwa wanafiki kwani ni wao walioipinga mwaka 2010.

Wakati huo huo Raila amesema marekebisho hayo ya katiba yanafaa kuurudisha utawala wa zamani kwa kulipa bunge nguvu zaidi huku akipendelea mawaziri wachaguliwe kutoka bungeni.

 Kuhusiana na kugombea urais mwaka 2022 Raila amesema kwa sasa wanachozingatia ni umoja wa kitaifa na wakati ukifika ataweka wazi swala hilo.

 

Show More

Related Articles