HabariMilele FmSwahili

“Acheni idara husika zibaini ukweli kuhusu ubadhirifu wa fedha za mabwawa”, asema Raila

Waruhusu maafisa waliotwikwa wajibu wa kukabili ufisadi kutekeleza wajibu wao. ndio kauli ya kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye ameendelea kupinga kauli ya naibu rais dkt William Ruto kuhusiana na madai ya kufujwa mabilioni ya fedha zilizotengewa mradi wa ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Aror kaunti ya Elgeiyo Marakwet. Raila anasisitiza kuwa ni idara husika tu zinazoweza kubaini ukweli kuhusiana na madai ya kuporwa shilingi bilioni 21.

Kinara wa ODM Raila Odinga amekana madai kuwa maafikiano yake na rais Uhuru Kenyatta yanalenga kumzuia naibu rais dkt William Ruto kutwaa uongozi wa taifa 2022. Katika mahojiano na  kituo cha redio cha Milele fm Raila amesema lengo lao lilikuwa kupunfguza joto la kisiasa nchini kwa manufaa ya wananchi. Amewasuta wanaoeneza madai kuwa kuamkuana na rais Kenyatta kumezua mtafaruku wa kisiasa katika chama cha Jubilee akiwataka kuwa wanafuki.

Show More

Related Articles