HabariMilele FmSwahili

Mhubiri David Owour anatarajiwa kuandikisha taarifa katika idara ya DCI leo

Mhubiri David Owour anatarajiwa kuandikisha taarifa leo na idara ya upelezi wa makosa ya jinai DCI kuhusiana na tuhuma za ulaghai dhidi yake. Mhubiri huo anatazamiwa kuhojiwa katika kituo cha polisi cha Kabete kuhusiana na tuhuma kuwa alitwaa kwa njia ya ulaghai umiliki wa jengo linalomilikiwa na aliyekuwa wakili Jane Muthoni, hapa jijini Nairobi. Familia ya Muthoni inadai alilaghaiwa hali iliyochangia kukabidhi huduma ya mhubiri Owuor jengo hilo. Tayari DCI imemhoji Lily Macharia mfuasi katika kanisa la Owuor anayedaiwa kuteuliwa na Muthoni kuwa mkurugenzi mwenza wa kampuni yake ya uwekezaji wa nyumba za makazi ya— Shaba investments limited

Show More

Related Articles