HabariPilipili FmPilipili FM News

Ukarabati Wa Bustani Ya Mama Ngina Umefikia Asilimia 40.

Ukarabati wa bustani ya Mama Ngina Kwa shughuli za utalii unaendelea huku wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwa wakitegemea bustani hiyo kwa biashara zao ndogo ndogo wakilalamikia kukosa shughuli za kujikimu.

Wafanyabiashara hao sasa wanaomba serikali kuwahusisha katika shughuli za kibiashara mradi huo utakapomalizika.

Rais Uhuru Kenyatta alitoa makataa ya hadi mwezi wa May Kukamilika.

Wanakandarasi katika mradi huo wanasema wamekamilisha asilimia arubaini ya mradi huo wakiwa na matumaini kuwa afikapo May utakuwa umemalizika.

Show More

Related Articles