HabariPilipili FmPilipili FM News

Mudavadi Amtaka Rais Kenyatta kuwachukulia Hatua Kali Wafisadi.

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi anamtaka rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha waliopora fedha za mabwawa wanachukuliwa hatua zifaazo kisheria akieleza kuwepo watu wanaopanga kuhujumu mipango hiyo.

Mudavadi aidha amewashtumu baadhi ya viongozi wanaoingilia utendakazi wa vitengo vya EACC na DCI vinavyo ongoza juhudi za kupambana na ufisadi  akisema nia yao ni kutatiza mchakato wa kusaka fedha  zilizopotea.

Kiongozi huyo anasema wanaolalama kuhusiana na ripoti za ufisadi inaonyesha wazi  huenda wanahusika katika sakata hizo.

Mudavadi hata hivyo amewataka wakuu wa vitengo vya kukabibilana na ufisadi kutolegeza kamba kuona kuwa washukiwa wanafikishwa mahakamani.

Show More

Related Articles