HabariMilele FmSwahili

KNEC yaongeza muda wa usajili wa watahiniwa wa KCPE na KCSE

Baraza la mitihani nchini KNEC limeongeza muda wa usajili wa watahiniwa wa mtihani wa KCPE na KCSE mwaka huu kwa muda wa juma moja. Baraza hilo limeongeza muda huo  uliotarajiwa kukamilika  tarehe 7 mwezi  huu hadi tarehe 15.KNEC  pia imewapa muda wa hadi tarehe 6 wanafunzi zaidi ya 370,000 ambao usajili wao ulifutuliwa mbali kwa kutumia stakabadhi bandia  wakitakiwa kuwasilisha stakabadhi halali na kujisajili upya.Ni ujumbe ambao tayari umewasilishwa kwa wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti tofauti ili kuwaafahamisha wazazi.

Show More

Related Articles