HabariPilipili FmPilipili FM News

Atwoli Amentaka Rais Kuwachukulia Hatua Wafisadi Serikalini.

Katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi nchini Francis Atwoli sasa anamtaka rais Uhuru Kenyatta kuwachukulia hatua wafisadi wanaofuja pesa za umma serikalini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya muungano wa chama cha wafanyikazi barani afrika awamu ya 30 huko nairobi, Atwoli amesema ufisadi umechangia pakubwa kuzorota kwa uchumi wa taifa , na kwamba ipo haja kuwachukulia hatua wahusika.

Atwoli pia ameeleza umuhimu wa kuhusishwa kwa miungano ya wafanyikazi katika masuala ya uhuru wa mataifa pamoja na demokrasia ya nchi za afrika.

Show More

Related Articles