HabariPilipili FmPilipili FM News

Wauguzi wamerudi kazini athibitisha Panyako

Katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini Seth Panyako amethibitisha kwamba wauguzi wamerejea kazini kwa sasa kufuatia agizo la mahakama alilopokea siku ya alhamisi wiki jana.

Panyako ameyasema hayo kupitia mahojiano ya moja kwa moja katika runinga ya K24 , Ikiwa ni siku moja tu baada yake na wenzake 3 wa chama cha wauguzi kuponea adhabu ya mahakama ya leba kutokana na wao kukiuka agizo la mahakama kuwataka kusitisha mgomo hapo awali.

Panyako hata hivyo ameeleza kugadhabishwa kwao kufuatia hatua ya serikali kushindwa kutekeleza mkataba wa makubaliano, ilihali pesa nyingi zimekuwa zikifujwa kwenye sakata mbalimbali za ufisadi ikiwemo kwenye wizara ya afya.

 

Show More

Related Articles