HabariPilipili FmPilipili FM News

Mashirika Yakutetea Haki Kupokea Msaada Kutoka Kwa Serikali Ya Kilifi.

Serikali ya Kaunti ya Kilifi hivi karibuni inalenga kuyasaidia mashirika yanayotetea dhulma zinazowakumba watoto wa kike kama njia moja yapo ya kupiga jeki maswala yanayofungamaba na mimba za mapema.

Akiongea wakati wa hafla ya kupeana zawadi kwa wanafunzi waliofanya vyema katika shule ya Lakewood Green Olive ilioko Wadi ya Tezo,naibu gavana kaunti hio Gedion Saburi anasema tayari serikali hio imeweka mikakati thabiti ya kufanikisha mazungumzo  na mashirika hayo ili kuona kwamba wanayapa nguzu Zaidi za kukabiliana na maswala hayo nyanjani.

Anasema kuacha shule kwa idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanapaswa kuwa shuleni kutokana na mimba za mapema na ajira miongoni mwa watoto wadogo imekuwa tatizo sugu katika sehemu nyingi za Kaunti hio jambo ambalo linapaswa kutatuliwa kwa haraka.

Hatua hii inajiri muda mfupi baada ya viongozi wa kisiasa na wale wakidini kuahidi kuja pamoja ili kuweka msimamo thabiti wa kuwaokoa wanafunzi ambao wamekuwa wakiacha masomo baada ya kupachikwa mimba.

Show More

Related Articles