HabariPilipili FmPilipili FM News

Milioni 300 Zahitajika Kuisafirisha Ferry Mpya Kutoka Uturuki Hadi Mombasa Asema Gowa.

Wakenya watahitajika Kulipa shilingi  milioni 300 zaidi ili kusaidia kuiwasilisha ferry mpya ambayo imekwama nchini Uturuki.

Haya yamefichuliwa na mkurugenzi wa shirika la ferry Bakari Gowa, wakati alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usafiri.

Katika kandarasi iliyotiwa saini Juni 27 mwaka wa 2015,serikali ilinunua ferry mbili zilizopaswa kuwasilisishwa nchini kufikia novemba 2016.

Hata hivyo ni ferry moja ya MV Jambo iliyowasilishwa kufikia mwezi julai 2017; Ferry ya pili ilikosa kuwasilishwa kutokana na agizo la mahakama katika kesi iliyowasilishwa kuzuia ununuzi wa ferry hiyo.

Show More

Related Articles