Swahili Videos

Benki kuu yajieleza : Wabunge wapinga kanuni za kutoa au kuweka Ksh. 1m

Gavana wa benki kuu ya Kenya, Patrick Njoroge ameelezea kamati ya bunge la kitaifa kuhusu fedha kwamba kanuni zilizoratibiwa kuhusu kule kuweka fedha au kutoa fedha taslimu kutoka benki ya kiasi kisichozidi shilingi milioni moja zitasalia kutekelezwa.
Njoroge anadai kuwa iwapo basi utazidisha kiwango hicho ni sharti uhakiki maelezo muhimu ili benki iwe katika nafasi nzuri kuweza kubainisha fedha hizo zinatoka wapi au zinaelekea kwa matumizi yepi ili kusaidia kuziba mianya ya ulanguzi wa fedha, ufadhili wa ugaidi na ufisadi.

Show More

Related Articles