HabariPilipili FmPilipili FM News

Kilio Cha Wanafunzi Kwa Serikali Kuhusu HELB

Serikali inaombwa kuja na njia mbadala kabla kuanza kutekeleza amri ya kuwataka wanafunzi waliochukua mikopo ya HELB kuanza kulipia deni hilo.

Wanafunzi hao kutoka vyuo mbali mbali vya mafunzo wanataka serikali kutimiza wajibu wa kutoa ajira kwa vijana kabla ya kuanza kuwashinikiza vijana kulipa.

Katibu mkuu wa muungano wa vyuo vya mafunzo anamtaka waziri wa ELIMU Amina Mohammed Kuelewa umuhimu wa mchango wa vijana katika maendeleo ya nchi.Wanafunzi hao sasa wanasema kauli ya waziri Amina inwatia wasi wasi vijana wengine ambao wana azma ya kuomba mikopo wa HELB.

Show More

Related Articles