HabariMilele FmSwahili

Wizara ya elimu yakanusha madai ya kutoa agizo la kukamatwa waliokwepa kulipa mikopo ya HELB

Wizara ya elimu imekanusha madai ya kutoa agizo la kukamatwa watu waliokwepa kulipia mikopo waliyopokea kutoka bodi ya elimu ya juu HELB licha ya kuajiriwa. Katibu wa elimu ya vyuo vikuu wizara hiyo Colleta Suda amesema serikali hainuii kutumia  mabavu katika kuhakikisaga kuwa deni wanalodaiwa watu hao la shilingi bilioni saba limelipwa. Hata hivyo Suda ametoa wito kwa waliochukua mikopo hiyo kuilipia kwa mujibu wa makubaliano waliyoafikia na HELB

Suda pia amevishauri vyuo vikuu vya umma kupunguza idadi ya wafanyikazi kutokana na kupunguka kwa ufadhili kutoka serikali.

Show More

Related Articles