HabariMilele FmSwahili

Joseph Kori mumewe Mary Wambui aachiliwa kutoka seli za polisi

Joseph Kori mumewe Mary Wambui mama aliyeuwawa kinyama na mke mwenza majuma 3 yaliyopita ameachiliwa kutoka seli za polisi. Taarifa zinaarifu kwamba Kori ambaye alikuwa anazuiliwa kaitka kituo cha polisi cha Gigiri aliachiliwa jana usiku mwendo wa saa 3 usiku. Polisi kituoni humo wanasema maafisa kutoka idara ya upelelezi walifika na kumtoa katika seli hilo kwa kile walisema wanahitaji kumuhoji zaidi. Hata hivyo inaarifiwa saa chache baadaye maafisa hao walirejea bila Kori japo na barua ya kuonyesha kori ameachiliwa huru. Jamaa za Mary Wambui zilikuwa zimeitisha kuachiliwa Kori ili kuruhusu mazishi ya mwanao. Mahakama Februari 13 iliagiza kuzuiliwa kwa Kori, dereva wa texi Michela Mathenge na mke mwenza anayetuhimiwa kumuuwa Mary Wambui, Judith Wangu kwa siku 14 ili kuruhusu uchunguzi kabla ya kurejea tena mahakamani februari  27.

Show More

Related Articles