HabariMilele FmSwahili

Mamake mshukiwa mkuu wa shambulizi la Dusit D2 Salim Gichunge ashtakiwa

Mama wa Ali Salim Gichunge, jamaa aliyepanga na kutekeleza shambulizi la Dusit D2 ameshtakiwa kwa kuficha serikali habari muhimu kuhusu mwanawe. Sakina Mariam Abdalla mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya ugaidi Francis Andayi, anadaiwa kati ya mwaka 2015 na 2019, alikuwa na ufahamu tosha kuhusu kupotea mwanawe japo hakuripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi. Upand wa mashtaka ukisema kukosa kuwasilishwa habaari hizo muhimu ndio kulichagia shambulizi hilo. Maafisa kutoka kitengo cha kukabili ugaidi aidha wameimba mahakama kumzuilia mariam kwa muda zaidi kwa misingi huenda akahitilafiana na uchunguzi. Idara hiyo pia imedokeza mahakamani kwamba washukwia zaidi wa shambulizi hilo lililopelekea vifo vya watu 21 watakuwa wanafikishwa mahakamani juma lijalo

Show More

Related Articles