HabariMilele FmSwahili

Wapenzi wa jinsia moja waelezea kutamaushwa na uamuzi wa mahakama kuhusu kesi yao

Ni pigo kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya mahakama kuu kwa mara nyingine kuhairisha hadi mwezi Mei 24 utoaji uamuzi wa kesi kuhusu uhalali wa uhusiano huo.  Jopo la majaji 3 akimewo Chacha Mwita limesema limekumbwa na changamoto ya kupata muda wa kuandika uamuzi wao. Ameomba radhi kwa pande husika katika kesi hiyo kwa niaba ya majaji wenza Roselyne Aburili, na John Mativo watatoa uamuzi anaosema kwa sasa wanashughulika kesi zingine.

Aidha umauzi huu umewatamausha washiriki wa uhusiano wakisema sio haki kwa kesi hiyo kushinda ikihairisha kesi hii ambayo wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu. Wanaharakati wanaotetea haki hiyo wameitaka mahakama kuamua kuhusu uhalali wa uhusiano wao. Kulingana na sheria ya sasa nchini, hukumu ya kutapatikana akihusika na mapenzi ya jinsi moja ni  miaka 14 gerezani

Show More

Related Articles