HabariMilele FmSwahili

Watu 3 wakamatwa kwa kuuza dawa bila idhini Nyanza

Watu watatu wamekamatwa huku maduka 73 ya kuuza dawa yamefungwa katika eneo la Nyanza baada ya kugundulika kuhudumu bila vibali kutoka bodi ya dawa na sumu nchini.  Kulingana na afisa wa uchunguzi katika bodi hiyo Dominic Kariuki maduka hayo yalitambulika kufuatia msako uliodumu siku 5 katika kaunti za Kisumu,Nyamira,Kisii,Homabay,Migori na Siaya . Kariuki amedhibitisha kuwa baadhi ya maduka yalikuwa yakiuza dawa zilizokuwa na nembo ya serikali kinyume na sheria.

Show More

Related Articles