HabariMilele FmSwahili

Jubilee yamuidhinisha Ahmed Kolosh kuwania ubunge Wajir Magharibi

Chama cha Jubilee kimemuidhinisha Ahmed Kolosh kuepeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Wajir Magharibi. Akimkabidhi tiketi hiyo Kolosh naibu rais dkt William Ruto ametangaza kuwa Jubilee kimejinadaa kunyakuwa ushindi katika kinyanganyiro hichio kutokana na umaarufu wake chama hicho katika kaunti hiyo.

Kolosh aliyepoteza kiti hicho baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali ushindi wake 2017 anatarajiwa kumenyana na prof. Yusuf Elmi wa ODM  katika uchaguzi mdogo wa Aprili 25.

Show More

Related Articles