HabariPilipili FmPilipili FM News

Kesi Kuhusu Uhalali Wa Mapenzi Ya Jinsia Moja Yahairishwa.

Mahakama kuu imeahirisha uamuzi uliokuwa unatarajiwa kuhusu uhalali wa sheria inayoharamisha mapenzi kwa watu wa jinsia moja hadi tarehe 24 ya mwezi mei mwaka huu.

Kwa mujibu wa jaji katika mahakama hiyo hii leo asubuhi, kesi hiyo imebidi iahirishwe kutokana na kuzidi kwa majukumu.

Chini ya sheria za Kenya, mapenzi ya jinsia moja ni hatia iliyo na hukumu ya miaka 14 gerezani.

Uamuzi huo utatolewa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na jaji Chacha Mwita.

Show More

Related Articles