Mediamax Network Limited

Wafadhili Wa Mradi Wa Mwache Kukaa Na Wakazi Kujadili Kuhusu Fidia.

Gavana  wa  kaunti  ya  Kwale  Salim Mvurya  amewataka  wasimamizi wa benki kuu ya dunia walio wafadhili wakuu wa mradi wa Mwache  kufanya vikao  na wakaazi wa eneo la Kasemeni huko Kinango watakaoathirika na mradi huo ili kuafikia makubaliano ya fidia.

Mvurya amesema hadi kufikia sasa  wenyeji bado hawana uhafamu wa kutosha unaohusiana na maswala ya fidia na uhamisho .

Hata hivyo ametoa  changamoto kwa wakaazi hao  kupatikana kwenye vikao ili kutoa dukuduku zao  kwa  wafadhili hao.

Mvurya amesisitiza kuwa mradi huo ni kwa manufaa ya wenyeji wa kwale  na wala sio wa kisiasa  kama inavyosambazwa na baadhi ya wanasiasa katika kaunti