HabariPilipili FmPilipili FM News

Wawekezaji Wa Utalii Watishia Kuishtaki Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi.

Hali ya kutofautiana imeibuka baina ya seikali ya kaunti ya Kilifi na wawekezaji wa utalii na maeneo ya burudani kuhusiana na sheria ya kudhibiti kelele.

Wadau hao wamesema sheria hiyo inawapinga kuendeleza shughuli zao na kutishia kuelekea mahakamani kupinga sheria hiyo.

Aidha wadau hao wamesema kupitishwa kwa sheria hiyo, imeathiri viwango vya watalii kuzuru maeneo hayo kwa asilimia 50 na kusema sheria hiyo inawapinga watalii uhuru wa kujivinjari.

Hivyo basi wameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kulegeza kamba kiasi ikizingatiwa serikali inapata kipato kupitia utali na wakaazi wengi wa Kilifi wana pata rizki zao kupitia sekta hiyo ya utalii.

 

Show More

Related Articles