HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Ya Mombasa Imeitisha Kikao Na Chama Cha Wauguzi.

Serikali ya kaunti ya Mombasa imeitisha kikao  na chama cha wauguzi ili kujadili hatima yao kuhusiana na marupurupu iliowalipa.

Haya ni kulingana na katibu mkuu wa chama cha wauguzi kaunti ya Mombasa Peter Maroko.

Akiongea na meza yetu ya habari Maroko amesema wameshtushwa na hatua ya tume ya mishahara SRC ya kutaka marupurupu waliyiolipwa na kaunti yarudishwe lakini wanatarajiwa watapata suluhu wakati wa mkutano huo.

Awali mkurugenzi wa mawasiliano kaunti ya Mombasa Richard Chacha alisema watakutana na muungano huo pamoja na wakuu wa SRC ili kutafuta suliuhu kuhusu marupurupu hayo.

 

 

 

 

Show More

Related Articles