HabariPilipili FmPilipili FM News

Mshukiwa Wa Ugaidi Aachiliwa Huru Na Mahakama Mombasa.

Mahakama ya Mombasa imemwachilia huru mwanamume mmoja anayekabiliwa na mashtaka kumi ya ugaidi. Hii ni  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha kufuatia madai hayo.

Yasri Azam Abdulakhan alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki bastola aina ya Glock, risasi tatu sawa na kumiliki vifaa vinavyotumika kutekeleza shughuli za kigaidi.

YASRI aidha anadaiwa kupatikana na simu, kadi za simu, compact discs na kadi ya SD card katika nyumba aliyokuwa akiishi na nduguye kwenye mtaa wa Majengo mapya Likoni Kaunti ya Mombasa mnamo tarehe 20 mwezi wa 9 mwaka 2016.

Akitoa uamuzi huo hakimu Henry Nyakwemba wa mahakama kuu ya Mombasa amesema ushahidi uliotolewa ni hafifu mno, kuthibitisha mashtaka yanayomkabili mshukiwa huyo.

Awali afisa wa upelelezi Bernard Mudavadi ameiambia mahakama hiyo kwamba walipata taarifa kuwa YASIR alikuwa akitarajia kupokea bunduki mbili aina ya AK47 kutoa nchini Somalia.

Show More

Related Articles