HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Afya Kuajiri Wauguzi

 

Wizara ya afya ikishirikiana na baraza la magavana imeamua kuajiri wauguzi  kwa mkataba, kufuatia mgomo wa wauguzi unaoendelea katika kaunti kumi. Mkataba huo utahakikisha kuwa shughuli zinaendeshwa kwa njia nzuri katika vituo vya afya ambapo wauguzi hao walidinda kufuata agizo la mahakama na hata maelekezo ya rais kurudi kazini. Hata hivyo,wametoa onyo kwa wauguzi wanaoenedelea kushiriki mgomo kufutwa kazi ,licha ya kukaidi amri ya rais wiki iliyopita.

 

Show More

Related Articles